Customer Care

Home > Personal  > Customer care > Help > Taarifa kwa Umma

TAARIFA KWA UMMA


Airtel Tanzania wanapenda kuwatangazia umma kwamba kuna tangazo linalozambazwa katika mitandao ya kijamii ikiwemo Whatsapp, Tangazo hilo si halali kwa sababu limeongezewa maneno yasiyo ya staha ambayo hayakuwemo kwenye Tangazo lililo andaliwa awali.


Airtel Tanzania inapenda kuomba radhi kwa yeyote aliye kwazika na kuwataarifu kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa kwa walioandaa tangazo hilo kwa kutumia nembo ya Airtel bila idhini.


Airtel Tanzania wanajali maadili na hawawezi kutumia lugha zisizo na staha kwenye kutangaza huduma na bidhaa zake.


Airtel mtandao bomba kwa smartphone yako.